Kenya kufungua robo fainali dhidi ya Algeria, Voliboli ya Afrika kwa vipusa

Fainali itasakatwa tarehe tano mwezi ujao huku mabingwa wakifuzu kushiriki mashindano ya dunia mwaka ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Kenya, Malkia Strikers, watafungua hatua ya robo fainali ya mashindano ya mpira wa wavu kwa wanawake barani Afrika Jumanne, Septemba Mosi dhidi ya Algeria katika ukumbi wa Kasarani.

Baadaye, Uganda watakumbana na Cameroon katika kwota fainali ya pili huku mshindi akiweka miadi dhidi ya atakayeshinda kati ya Kenya na Algeria kwenye nusu fainali ya Septemba 3.

Rwanda watamenyana na Ghana katika robo fainali ya tatu huku Misri wakihitimisha ratiba dhidi ya Tunisia, ambapo washindi watakabiliana katika nusu fainali ya pili Septemba 4.

Fainali itasakatwa tarehe tano mwezi ujao huku mabingwa wakifuzu kushiriki mashindano ya dunia mwaka ujao.

Share This Article