Harambee Stars itafungua harakati za kuwania kombe la Mapinduzi kesho dhidi ya Burkinafaso nchini Zanzibar.
Kenya inayonolewa na kaimu kocha Francis Kimanzi iliwasili kisiwani Zanzibar jana jioni kwa mashindano hayo na kufanya mazoezi ya kwanza.
Mashindano hayo yatakuwa pia maandalizi ya mwisho mwisho kwa Kenya kwa makala ya nane ya fainali za CHAN nchini Kenya,Uganda na Tanzania.