Kenya inaunga mkono vita dhidi ya uhalifu wa kimataifa, asema Murkomen

Waziri ametoa wito wa kuharakishwa kwa ushirikishanaji wa habari za kijasusi kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni, na ushirikiano thabiti wa sekta ya umma na kibinafsi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen.

Kenya inaunga mkono kuimarishwa kwa ushirikiano katika kukabiliana na ulaghai wa kimataifa, makundi ya wahalifu na kulinda uadilifu wa mifumo ya kifedha na kidijitali.

Akizungumza Jijini Vienna, Austria wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu ulaghai wa mwaka 2026, Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen alitoa wito wa kuharakishwa kwa ushirikishanaji wa habari za kijasusi kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni, ushirikiano thabiti wa sekta ya umma na kibinafsi, uwekezaji endelevu, utoaji mafunzo na ubadilishanaji wa teknolojia.

“Kenya imeidhinisha rasmi vita dhidi ya ulaghai na ushirikiano wa sekta za umma na zile za kibinafsi kukabiliana na ulaghai na imejitolea kuimarisha ushiriki wake katika operesheni za kimataifa dhidi ya uhalifu wa mtandaoni,” alisema Murkomen.

Aidha, alidokeza kuwa Kenya imejitolea kushirikiana na washirika wengine kuboresha ushirikiano wa kikanda, kuwiainisha sheria za uhalifu wa mtandaoni na kuunga mkono mkakati wa kikanda wa ushirikishanaji wa habari za kijasusi kuhusu ulaghai.

Alisema kuwa ukuaji wa dijitali unasalia kuwa nguvu ya ufanisi, ujumuishaji na fursa kwa wananchi.

Share This Article