Kenya iko tayari kuandaa fainali za mwaka huu za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanandinga wanaopiga soka Afrika maarufu kama CHAN.
Haya yalisemwa siku ya Alhamisi na Waziri wa michezo Ababu Namwamba alipokutana na katibu mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Verone Omba katika mkahawa wa Pride Inn Paradise kaunti ya Mombasa.
Katibu Mkuu wa CAF yuko nchini kuhudhuria kikao cha muungano wa vyama vya soka Afrika mashariki na ya kati CECAFA .
Kenya itaandaa fainali za CHAN mwezi Septemba mwaka huu.
Fainali za CHAN huandaliwa kila baada ya miaka miwili.