Kenya Airways yaongeza hadi mbili kwa siku safari zake kwenda London

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la ndege la Kenya Airways, KQ limeongeza safari zake kutoka Nairobi hadi London hadi mbili kwa siku.

KQ imekuwa na safari moja pekee kwa siku kutoka Nairobi hadi London.

Katika taarifa, shirika hilo linasema safari hizo mbili kwa siku kwenda London zitaanza rasmi Oktoba 29 kwa kutumia ndege za KQ 102 na KQ 100.

KQ itatumia ndege ya Boeing 787 Dreamliner katika safari hiyo mpya na kufikisha idadi ya safari 14 za ndege zinazosafiri kutoka Nairobi hadi London kwa wiki kutoka 10 za awali.

Share This Article