Kenya Airways yanakili faida ya shilingi bilioni 5.4

Tom Mathinji
1 Min Read
Ndege ya shirika la Kenya Airways.

Shirika la ndege la Kenya Airways, limenakili faida ya shilingi bilioni 5.4, baada ya ushuru katika kipindi kilichokamilika Disemba 31, 2024.

Shirika hilo lilisema faida hiyo ambayo ni ongezeko la asilimia 124 kutoka hasara ya shilingi bilioni 22.7 mwaka 2023, lilitokana na idadi kubwa ya wasafiri katika kipindi hicho.

“Mafanikio haya yameleta mabadiliko makubwa katika shirika hili, yanayozingatia huduma bora kwa wateja, operesheni zilizoimarika, nidhamu ya kifedha na uvumbuzi,” alisema mwenyekiti wa shirika hilo Michael Joseph.

Kulingana na mwenyekiti huyo, shirika hilo pia lilinakili faida ya asilimia 58 katika shughuli za operesheni, ambayo iliongezeka hadi shilingi bilioni 16.2 ikilinganishwa na faida ya shilingi bilioni 10.5 zilizonakiliwa mwaka 2023.

Wakati huo huo Joseph alisema kuimarika kwa shilingi ya Kenya, kumesababisha mazingira bora ya operesheni za shirika hilo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *