KeNHA yafungua tena barabara kuu ya Nakuru-Eldoret

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya usimamizi wa barabara kuu nchini, KeNHA, imetangaza kufungua barabara kuu ya Nakuru–Eldoret.

Hii ni baada ya barabara hiyo kufungwa kwa muda.

Barabara hiyo ilikuwa imefungwa baada ya kuharibiwa na mvua.

Aidha, KeNHA imetangaza kuwa usafiri wa kawaida wa magari na watu umerejelewa kwenye barabara hiyo.

Barabara hiyo ilikuwa imefungwa karibu na mzunguko wa makutano karibu na kampuni ya Eveready.

Kufungwa kwa barabara hiyo kulisababisha msongamano mkubwa wa magari.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article