Mamlaka ya barabara kuu nchini KENHA imetangaza kufunga barabara ya B115 kati ya Ruiru,Tatu City hadi Kiambu kaunzia Jumatatu ijayo disemba 23 hadi Januari 6 mwaka ujao.
KENHA badala yake imewataka wenye magari kutumia barabara mbadala.
Barabara hiyo itafungwa kuanzia kwa makutano ya Kirigiti-Ruiri stage hadi Kiambu mjini.
KENHA itafunga barabara hiyo kuanzia Jumatatu saa kumi na mbili jioni ili kupisha ukarabati.
Wasafiri wameagizwa kutumia barabara mbadala ya Kirigiti-Ruiru stage junction,na Kiambu Town wakati wote wa ukarabati huo.