KeNHA yafunga barabara ya Kenol-Sagana

Dismas Otuke
0 Min Read

Mamlaka ya barabara kuu nchini (KeNHA)imetangaza kufunga sehemu ya barabara ya Kenol – Sagana baada ya kuharibiwa na mvua.

Ililazimu barabara hiyo kufungwa kufuatia kujaa kwa vifusi vya mawe vinaporomoka kutoka kwa mlima ulio karibu na eneo la Mugetho.

KeNHA imewashauri madereva kutumia kwa pamoja mzunguko wa Sagana kwa makini na kufuata maelekezo ya polisi wa trafiki.

Mamlaka hiyo imeahidi kujitahidi kurejesha hali ya kawaida.

TAGGED:
Share This Article