KEMSA yampongeza Waziri wa Afya mteule Dkt. Deborah Barasa

Tom Mathinji
1 Min Read
Kemsa yampongeza Dkt. Debora Barasa.

Mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu hapa nchini KEMSA, imempongeza Dkt. Deborah Mlongo Barasa kufuatia uteuzi wake kuwa Waziri wa Afya.

Siku ya Ijumaa Rais Ruto alitaja nusu ya kwanza ya Baraza jipya la Mawaziri, akisema ameanza mchakato wa kubuni Baraza jumuishi la Mawaziri.

Kupitia kwa taarifa iliyotiwa saini na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka hiyo Irungu Nyakera, KEMSA ilimtaja Dkt. Barasa kuwa mwenye tajiriba ya miaka 15 katika ya utabibu,huku akiwa na utaalma wa magonjwa ya kuambukiza na matibabu ya ndani ya mwili.

“Ametekeleza majukumu muhimu katika sekta ya afya, ikiwa ni pamoja na kushughulikia magonjwa yaliyozuka,” ilisema KEMSA.

Aidha mamlaka hiyo ilisema inalenga kushirikiana na Dkt. Barasa kutimiza malengo yake ya usambazaji wa dawa na vifaa vya matibabu kwa zaidi ya vituo 15,000 vya afya kote nchini.

Dkt Barasa pia amewahi kuwa mshauri wa magonjwa ya ndani ya mwili katika Shirika la Afya duniani WHO.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article