Mbunge wa zamani wa eneo la Mugirango Magharibi Vincent Mogaka Kemosi aliteuliwa kuwa balozi na Rais William Ruto hata baada yake kukataa kazi hiyo.
Uteuzi wa mabalozi ulitangazwa na Rais kupitia gazeti rasmi la serikali Mei 3, 2024 ambapo Mogaka ni mmoja wa waliofaulu baada ya usaili bungeni.
Kemosi aliteuliwa kuwakilisha Kenya jijini Accra nchini Ghana na aliandika barua kwa kamati ya bunge iliyohusika na usaili akisema kwamba hangefika kwa usaili.
Alitaja sababu za kibinafsi kuwa kichochezi kikuu kwake kukataa kazi hiyo.
Inasubiriwa kuona iwapo Kemosi atakwenda Ghana kwa kazi hiyo.