KCB na Mathare United wamesajili ushindi katika mechi za ligi Kuu zilizosakatwa Jumamosi katika mechi za mzunguko wa saba .
Mathare United wamesajili ushindi wa pili baada ya kuwalemea Talanta FC mabao 2-0.
Certic Asango na Ellie Asieche wamefunga goli moja kila mmoja kwa vijana wa Mathare .
Kcb iliwalemea Tusker Fc mabao 3-2,Francis Kahiro alipachika mabao kwa KCB huku James Kinyanjui akiongeza moja.
Ryan Ogam alipachika magoli mawili ya Tusker FC.
Shabana FC wamelazimisha sare ya bao 1 dhidi ya Kariobangi Sharks.