Kaunti zanufaika pakubwa na maeneo ya Ustawi wa Viwanda

Shilingi milioni 500 zimewekezwa kwa pamoja katika kaunti 34 zinazoshiriki mpango huo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kaunti zanufaika pakubwa na maeneo ya ustawi wa viwanda.

Uwekezaji wa shilingi bilioni 8.5 katika maeneo ya Ustawi wa Viwanda kwenye kaunti, umeimarisha pakuwa ukuaji wa kaunti kupitia upatikanaji wa nafasi za ajira, ubunifu na mageuzi ya kiuchumi.

Rais William Ruto amesema kupitia ushirikiano wa karibu kati ya serikali ya taifa na zile za kaunti, shilingi milioni 500 zimewekezwa kwa pamoja katika kaunti 34 zinazoshiriki mpango huo, na kuweka msingi wa ukuaji wa viwanda kuanzia maeneo ya mashinani.

“Hatua hiyo itawawezesha wakulima, kuwasaidia wazalishaji bidhaa, kuimarisha biashara za ndani, na kuleta utajiri katika kaunti zote,” alisema Rais Ruto.

Rais alisema  shilingi bilioni 2.4 zitawekezwa katika vifaa vya watumiaji wa kawaida katika mpango huo maalum  huku takriban shilingi milioni 150 zikitengwa kwa kila kituo ili kusaidia vipaumbele vya kuongeza thamani katika kila kaunti.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo leo Alhamisi  katika Ikulu ya Nairobi, aliposhuhudia kutiwa saini kwa makubaliano ya kubuni maeneo ya viwanda katika kaunti.

TAGGED:
Share This Article