Kaunti ya Kilifi kuanzisha kituo cha matibabu ya Saratani

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali ya kaunti ya Kilifi inajiandaa kuanzisha kituo cha kutibu ugonjwa saratani, ili kupunguza mzigo wa wagonjwa wa saratani kutafuta matibabu katika mataifa ya nje.

Serikali ya kaunti hiyo inatarajiwa  kupokea vifaa vya saratani kupitia ushirikiano na shirika moja kutoka taifa la  Austria mjini Vienna.

Gavana kaunti ya  Kilifi Gideon Mung’aro alikuwa ametafuta usaidizi kwa shirika hilo alipozuru taifa hilo mwaka jana. Kwa mijubu wa gavana huyo, tayari serikali ya kitaifa imeidhinisha kituo hicho ambacho kinasubiri tu kupokea vifaa.

Akiongea katika hospitali ya chuo kikuu cha Thumbay  katika taifa la Milki za kiarabu mjini  Dubai wakati wa ziara rasmi ya kuwapeleka maafisa wa huduma za matibabu kwa mpango wa ushirikiano wa kutoa mafunzo katika chuo kikuu, Mung’aro alisema kuwa kituo hicho kitawawezesha wagonjwa kupata matibabu ya gharama nafuu katika eneo la pwani.

Mung’aro alisema pia ameshirikiana na hospitali ya chuo kikuu cha Thumbay ambacho kinatoa huduma bora za matibabu hasa matibabu ya ugonjwa wa saratani ili kuwezesha wafanyikazi wa huduma za matibabu kupokea mafunzo mwafaka ya kuwashughulikia wagonjwa wa saratani.

Share This Article