Kaunti saba kukosa umeme Alhamisi

Dismas Otuke
1 Min Read

Kaunti saba nchini zinatarajiwa kukosa umeme leo kulingana na arifa kutoka kwa kampuni ya kusambaza umeme nchini, KPLC.

Maeneo kadhaa ya kaunti za Nairobi, Bomet, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet, Kirinyaga, Meru na Kiambu yatakosa nguvu za umeme.

Katika kaunti Nairobi, maeneo ya  Ridgeways, Safari Park Hotel, Jambo Grill, Milele, Sunstar Hotel na Top Quality Garage yatakumbwa na ukosefu wa umeme.

Kule Bomet, maeneo ya Siongiroi na Labotiet yataathirika kwa kupotea kwa umeme, huku Endebes na Panocal yakikumbwa na tatizo hilo huko Trans-Nzoia.

TAGGED:
Share This Article