Kaunti 5 zinazoongoza kwa usajili wa SHA

Martin Mwanje
1 Min Read
Anne Waiguru - Gavana wa Kirinyaga inayoongoza katika usajili wa SHA

Rais William Ruto amezilimbikizia sifa kaunti tano zinazoongoza kwa usajili wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) inayosimamiautekelezaji wa Bima ya Afya ya Jamii, SHIF, maarufu kama Taifa Care. 

Wakenya milioni 16.6 wamejisajili kwenye mpango huo uliozinduliwa Oktoba mosi mwaka huu.

Rais Ruto anasema Wakenya milioni 5.6 walihamishwa kutoka iliyokuwa Hazina ya Bima ya Kitaifa ya Afya, NHIF huku wengine milioni 11 wakijisajili kwenye mpango huo miezi miwili tangu kuzinduliwa kwake.

Kaunti ya Kirinyaga yake Gavana Anne Waiguru inaongoza jedwali la kaunti zilizoandikisha idadi kubwa ya watu kwenye mpango wa SHA.

Inafuatwa na kaunti za Nyeri, Bomet, Embu na kisha Lamu.

“Hii inamaanisha kuwa, katika kipindi tu cha miezi miwili, Wakenya milioni 11 ambao awali walikosa huduma za matibabu sasa wamejisajili, huku mchakato wa kujisajili ukiendelea kwa kishindo kila sehemu ya nchi,” alisema Rais Ruto wakati akiliongoza taifa kuadhimisha Sikukuu ya Jamhuri katika bustani ya Uhuru Gardens.

“Taifa Care huhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa raia wote waliojisajili bila ubaguzi wa aina yoyote.”

Rais Ruto amewataka Wakenya kujiandikishwa kwa wingi kwa SHA ili kuhakikisha wanapata huduma bora za matibabu.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *