Katibu wa Kilimo akutana na wadau wa chai kuharakisha mageuzi ya sekta

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu katika Wizara ya Kilimo Kiprono Ronoh, amekutana na wadau wa chai nchini siku ya Jumatatu katika juhudi za kuharakisha mageuzi katika sekta hiyo.

Ronoh amejadiliana na wadau wa setka hiyo kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto zilizopo, kutafuta soko na kuboresha viwango vya uzalishaji zao hilo.

Aidha, wadau walielezea haja ya kuwekeza zaidi katika utafiti, ili kuimarisha chai inayokuzwa na kukidhi mahitaji ya soko la kimataifa.

Pia walizungumza kuhusu mbinu zilizowekwa na wakulima kuongeza faida katika kilimo cha chai, mbinu za ushirikishwaji na utendakazi kwa wakulima wote.

Mageuzi yanayolengwa yanaangazia kuweka Kenya, sawa na soko la kimataifa na mageuzi ya ulimwengu kuhusu zao hilo na kuinua hadhi ya wakulima.

Website |  + posts
Share This Article