Katibu wa Chama tawala nchini China Li Xi, yuko humu nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu na anatarajiwa kukutana na Rais William Ruto kwa mazungumzo ya pande mbili.
Xi aliyewasili jana alilakiwa na waziri aliye na mamlaka makuu Musalia Mudavadi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Xi anatarajiwa pia kukutana na viongozi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kujadili njia za kuimarisha ushirikiano kati ya chama cha kikomunisti cha China (CPC) na cha UDA kwa ajili ya kuimarisha huduma za vyama hivyo vya kisiasa kwa raia.
Xi ni mwanachama wa kamati kuu simamizi ya chama cha kikomunisti cha China (CPC) na katibu wa tume ya ukaguzi wa nidhamu ya chama hicho.
Ziara yake imewadia wiki chache baada ya mkutano wa ushirikiano kati ya China na Afrika kukamilika nchini China.