Klabu ya Bayer Leverkusen imemteua aliyekuwa kocha wa Denmark, Kasper Hjulmand kuwa meneja mpya kwa mkataba wa miaka miwili.
Ni mara ya kwanza kwa Hjulmand kufanya kazi ya ukufunzi wa soka tangu mwaka 2019.
Meneja huyo anatarajiwa kuanza kutekeleza majukumu yake Ijumaa hii katika mechi dhidi ya Eintracht Frankfurt.