Uwanja wa kimataifa wa Kasarani umefungwa kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kufanyiwa ukarabati kwa maandalizi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027.
Akitoa tangazo hilo Ijumaa Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amesema kuwa kampuni ya China imepewa kandarasi hiyo na itasimamiwa na jeshi la Kenya.
Namwamba ameongeza kuwa ukarabati utafanyiwa viti,vyoo ,vyumba vya kubadilisha nguo,na taa .
Serikali pia imetangaza kufungua uwanja mpya wa Talanta Hela hivi karibuni ambao pia utatumika kuandaa mechi za AFCON mwaka 2027.
Kuhusu mashindano ya Riadha ya Kip Keino Classic,Waziri Namwamba amasema wanashauriana na chama cha Riadha Kenya kuhusu uwanja mbadala.
Mashindano ya Kip Keino Classic yameratibiwa kuandaliwa April 10 mwaka ujao.
Kenya iliteuliwa kuandaa mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa Pamoja na Tanzania na Uganda .