Karua ashutumu bunge kwa kumbandua Gachagua

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amesema ameshutumu bunge kwa kutumika vibaya, kufuatia hatua yake ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Karua amesema iansikitisha kuona kuwa kumewa na mauaji mengi ya kiholela ya waandamanaji wa amani pamoja na utekaji nyara bila kupata haki na bunge lilishindwa kuwajibika.

Karua ameelezea hofu yake kuhusu mchakato unaoendelea wa kumtimua naibu Rais kuwa njama ya kuficha mambo mengi yanayowaumiza Wakenya, ikiwemo bima mpya ya SHIF iliyo na changamoto tele,mfumo wa ufadhili elimu.

Badala yake amelitaka bunge kuwajibika na kupitisha sehria na hoja zinazowasaidia Wakenya wote bali sio kutumika kwa maslahi ya kibinafsi.

Amewataka Wakenya kusimama imara na kuitetea na kuilinda katiba ya Kenya .

Website |  + posts
Share This Article