KANU yamteua Moi kuwania Useneta Baringo

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha KANU kimemteua Mwenyekiti wake  Gideon Moi, kuwa mgombeaji wake wa Useneta wa Baringo kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuandaliwa  Novemba 27 mwaka huu.

Baraza kuu la KANU limekutana Alhimisi na kumteua Moi kuwa mpeperushaji bendera wake kwenye uchaguzi huo mdogo.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha William Cheptumo Februari 16 mwaka huu.

Moi anawania kiti hicho kwa muhula wa pili baada ya kuhudumu kwa muhula wa kwanza kati ya mwaka  2017 hadi 2022 alipshindwa na marehemu Cheptumo.

 

Website |  + posts
Share This Article