Kansela wa Ujerumani apoteza kura ya imani

Martin Mwanje
1 Min Read
Olaf Scholz - Kansela wa Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz jana Jumatatu jioni alipoteza kura ya imani iliyopigwa katika bunge la nchi hiyo. 

Hatua hiyo inatoa fursa ya bunge la nchi hiyo kuvunjwa na uchaguzi wa ghafla kuandaliwa mwakani.

Jumla ya wabunge 394 kati ya 717 wa Bunge la Taifa, linalojulikana kama Bundestag,  walipiga kura ya kutokuwa na imani na
Scholz.

Ni wabunge 207 pekee waliomuunga mkono.

Kura hiyo inatokana na kusambaratika kwa muungano wake wa vyama vitatu mwezi Novemba kulikosababishwa na hatua ya Scholz kumpiga kalamu Waziri wake wa Fedha kutoka chama mshirika cha FDP.

Hatua hiyo ilitokana na mivutano juu ya namna ya kufadhili bajeti ya mwaka ujao.

Serikali ya Scholz  imekuwa ikiyumbayumba kwa muda wa miezi kadhaa.

Scholz aliitisha kura hiyo kwa lengo la kushinikiza uchaguzi wa ghafla na kwa wakati huu,
amemwomba Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmier kuidhinisha rasmi
mpango huo.

Uchaguzi huo sasa unatarajiwa kufanyika Februari 23 huku upinzani unatazamia kubuni serikali mpya.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *