Kanja: Usalama utaimarishwa kwa wakazi na wanabiashara wa Tatu City

Tom Mathinji
1 Min Read

Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja, amesisitiza kujitolea kwa serikali kuhakikisha usalama wa wakazi na biashara katika eneo la Tatu City, ambalo limeshuhudia ongezeko la maendeleo.

Akizungumza alipozuru Tatu City,ambayo inajivunia zaidi ya biashara 80, Kanja alielezea umuhimu wa kuanzishwa kwa kituo cha polisi il kushughulikia mahitaji yanayoongezeka ya kiusalama.

“Tatu City ni nguzo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Kenya, na tunatambua umuhimu wa usalama kuhakikisha mradi huo unafanikiwa,” alisema Kanja.

Huku idadi ya watu inavyoongezeka Tatu City na viunga vyake, hitaji la kuwa na suluhu za kiusalama limekuwa muhimu zaidi.

Kwa sasa Tatu City ni nyumbani kwa familia 3,000 families, wanafunzi 4,500 na wafanyakazi 20,000 na kuifanya kuwa eneo kubwa zaidi la maendelo hapa nchini.

Kwa upande wake naibu Inspekta jenerali wa polisi Eliud Kipkoech Lagat, alisema atahakikisha maafisa wa polisi wa kutosha wanapelekwa katika kituo kidogo cha polisi kitakachobuniwa Tatu City.

Share This Article