Wakenya Justus Kangogo, Asbel Rutto, na Stanley Kurgat watashiriki makala ya 42 ya mbio za Vienna City Marathon, zitakazoandaliwa kesho nchini Austria.
Kangogo anajivunia muda bora wa saa 2:05:57, wakati Rutto, akiwa na muda wa 2:06:24, aliosajili katika ushindi wa Rome Marathon mwaka jana, ilihali Kurgat ana muda wa kasi wa saa 2 dakika 7 na sekunde 5.
Wakenya wengine watakaotimka mbio hizo ni pamoja na Douglas Chebii, Benard Kimeli, Bernard Muia, Mica Cheserek, Kipsambu Kimakal, Geoffrey Koech, Charles Ndiema, Edward Koonyo, Evans Yego na
Henry Kichana.
Zaidi ya wanariadha 45,000, wamejiandikisha kushiriki huku 13,000, wakijisajili kwa mbio za kilomita 42.