Kamworor kuongoza orodha ya Kenya mbio za Rotterdam

Radio Taifa
1 Min Read
Mwanariadha Geoffrey Kamworor

Bingwa mara mbili wa mbio za marathoni za New York Geoffrey Kamworor ataongoza orodha ya wanariadha mashuhuri watakaoshiriki makala ya mwaka huu ya mbio za Rotterdam.

Mbio hizo zitaandaliwa tarehe 13 mwezi huu.

Kamworor anashikilia muda bora wa kibinafsi wa saa 2, dakika 4 na sekunde 23, aliyouweka katika mbio za  marathoni za London Marathon mwaka 2023.

Mwanariadha huyo alimaliza wa pili katika mbio za Nusu Marathon za mwezi Februari mwaka huu , nyuma ya Jacob Kiplimo wa Uganda.

Bashir Abdi wa Ubelgiji anashikilia rekodi ya kozi mbio za marathoni za Rotterdam ya saa 2 dakika 03 na sekunde 36 iliyowekwa mwaka 2021.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *