Kampuni za Slovenia zakaribishwa kuwekeza nchini Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlka Makuu Musalia Mudavadi, ashauriana na naibu Waziri Mkuu wa Slovenia Tanja Fajon.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, ametoa wito kwa kampuni za Slovenia kutumia fursa zilizopo hapa nchini za utengenezaji bidhaa katika maeneo maalum ya bidhaa za kuuzwa nje ya nchi (EPZ) na pia katika maeneo maalum ya kiuchumi (ESZ).

Mudavadi aliyasema hayo leo Jumanne aliposhiriki mazungumzo na naibu Waziri Mkuu aliyepia waziri wa Mambo ya Nje na maswala ya bara Uropa wa Slovenia Bi. Tanja Fajon, aliyemtembelea afisini mwake Jijini Nairobi.

“Mazungumzo yetu yaliangazia ushirikiano katika sekta muhimu zikiwemo; biashara, mazingira, kawi safi, habari na mawasiliano na Mabadiliko ya Tabia Nchi,” alisema Mudavadi.

Mudavadi aliyepia waziri wa Mambo ya Nje, alisema katika mazungumzo hayo, walikubaliana kuimarisha juhudi za kupunguza uchafuzi wa hewa kwa kuboresha mazingira.

“Tumekubaliana kufanya kazi pamoja, hasaa katika kongamano lijalo la COP 29, ili kushinikiza mabadiliko zaidi na ujumuishaji wa ufadhili  wa mikakati ya kukabiliana na Tabia Nchi,” alidokeza Mudavadi.

Website |  + posts
Share This Article