Kampuni za kuuza ardhi zaonywa dhidi ya ulaghai

Tom Mathinji and Radio Taifa
1 Min Read
Waziri wa Ardhi Alice Wahome.

Waziri wa ardhi Alice Wahome, ameagiza bodi ya udhibiti wa mawakala wa ardhi EARB, kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ardhi, zinazowalaghai wanunuzi wa ardhi wasio na ufahamu.

Wahome pia ameagiza bodi hiyo kubuni sera zitakazohakikisha utatuzi wa haraka wa masuala ya kinidhamu yanayohusisha kampuni laghai au zinazojihusisha katika ukiukaji wa sheria.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa mkakati wa bodi hiyo, Wahome alifichua kwamba wizara yake ilikuwa ikifanya kazi na mashirika ya upelelezi kuongeza juhudi za ufuatiliaji wa kampuni za uuzaji ardhi, ili kuepusha kampuni hizo kutumika utakatishaji wa fedha na ugaidi.

Alielezea kujitolea kwa serikali katika kusaidia sekta ya ardhi kupitia mfumo bora wa ushuru utakaohakikisha uelekezaji wa manufaa kwa wanunuzi.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article