Kampuni ya ndege ya Uganda yazindua safari za moja kwa moja hadi London

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya ndege nchini Uganda imezindua safari za moja kwa moja kutoka Entebe hadi jijini London, Uingereza, kuanzia Mei 18 mwaka huu.

Ni mara ya kwanza kwa safari za moja kwa moja kutoka Uganda hadi London, baada ya shirika la ndege la Uingereza kusitisha safari hizo Julai mwaka 2015.

Safari za Entebbe hadi London ni mojawapo wa safari ndefu za shirika la ndege Uganda baada ya zile za Entebbe hadi Dubai na Entebbe hadi Mumbai.

Website |  + posts
Share This Article