Kampuni ya mafuta ya Shell imetangaza faida ya dola za Marekani bilioni 6 nukta 2, kati ya mwezi Julai na Septemba mwaka huu .
Wasimamizi wa Shell wanasema faida hiyo imetokana na kuongezwa kwa bei ya bidhaa za petroli katika soko la kimataifa kutokana na vita Urusi na Ukraine.
Faida ya mwaka huu ni ongezekeo la asilimia 23, kutoka kwa faida iliyonakiliwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu.