Mwimbaji wa nyimbo za injili Kambua, ametimiza umri wa miaka 40 na hangeficha furaha yake.
Alichapisha picha za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo alisema amefikisha miaka 40 huku akishukuru Mungu kwa kumpigania kila wakati.
“Niliponea mwongo ambao karibu univunje kabisa na ulitishia kunimaliza, lakini Mungu.” aliandika mwimbaji huyo na kuongeza kwamba yeye ni kielelezo cha agano la majaribi na ushindi.
Inaaminika kwamba alikuwa akizungumza kuhusu kipindi cha miaka 10 alichokaa kwenye ndoa bila kufanikiwa kupata mtoto lakini Mungu akambariki na mtoto baadaye.
Kambua anasema pia kwamba mwaka huu wa 40 wa maisha yake, anatarajia makuu kutoka kwa Mungu akisema hatakubali lolote ila lile alilotengewa na Mungu pekee.
“Maono yangu yako wazi sasa kuliko awali, Mungu ninasema ndio hata sasa, Ndio kwa njia zako, ndio kwa mapenzi yako. Ndio kwa wakati wako.” aliandika Kambua kwenye akaunti yake ya Instagram.
Aliendelea kukiri kwamba amani ya Mungu ndiyo amani yake, furaha ya Mungu ndiyo furaha yake, uwezo wa Mungu ndio uwezo wake na ndio ya Mungu ndio yake.
“Yesu asanye kwa safari iliyonifikisha miaka 40 na asante kwa safari itakayoniongoza.” alimalizia Kambua.