Kambi ya kijeshi nchini Iraq inayowahifadhi wanamgambo wanaoiunga mkono Iran imeharibiwa katika mlipuko, na kuuwa mtu mmoja na kujeruhi wanane, maafisa wa usalama wamesema.
Jeshi la Iraq halikuripoti ndege zisizo na rubani wala ndege za kivita katika eneo hilo kabla au wakati wa mlipuko huo.
Lakini kundi la wanamgambo lililohusika, Popular Mobilisation Forces (PMF), lililaumu shambulio hilo.
Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na mvutano kati ya Israel na Iran.
PMF ni shirika ambalo lina wanamgambo kadhaa wanaounga mkono Iran ambao ni sehemu ya mtandao wa washirika ambao Tehran imeweza kuwatumia kuendeleza maslahi yake katika Mashariki ya Kati kwa miaka.