Kamati ya masuala ya jinsia kuzinduliwa leo

Marion Bosire
1 Min Read

Wizara ya masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo inapanga kuzindua kamati ya masuala ya jinsia na utekelezaji hii leo, Jumatatu Novemba 25, 2024.

Hafla hiyo itaongozwa na waziri wa masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo Kipchumba Murkomen, na inapangiwa kuandaliwa katika jumba la Talanta Hela kuanzia saa mbili asubuhi.

Kamati hiyo imejukumiwa kuimarisha usawa wa kijinsia na kulinda haki za kila mmoja anayehusika katika sekta za vijana, michezo na ubunifu.

Lengo lake ni kutoa mwongozo wa kisera wa kuimarisha mazingira jumuishi na salama kwa washirika wote wa sekta hizo.

Website |  + posts
Share This Article