Kamati ya Fedha ya Seneti yazuru Kakamega

Martin Mwanje
1 Min Read
Kamati ya Fedha ya bunge le Seneti jana Jumatatu ilizuru kaunti ya Kakamega kutathmini hali ya madeni inayodaiwa kaunti hiyo na ikiwa miradi mbalimbali imetekelezwa kikamilifu. 
Ikiongozwa na Seneta wa Mandera Ali Roba, kamati hiyo aidha ililitembelea bunge la kaunti hiyo na kufanya kikao na wawakilishi wadi.
Iliuhakikishia umma kuwa ziara hiyo haijachochewa kisiasa.
Baadaye, ilikagua barabara ya Chebuyusi-Navakholo kutathmini hatua iliyopigwa katika ujenzi wake na ustahiki wa fedha zilizotengewa ujenzi wake kabla ya kukutana na Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa kutafuta majibu ya maswali yao.
Gavana Barasa aliwahakikishia madeni inayodaiwa kaunti hiyo yatalipwa na kukanusha madai ya kushamiri kwa ubaguzi katika utoaji wa zabuni kwa wanakandarasi.
Hata hivyo, Seneta wa kaunti ya Kakamega Dkt. Boni Khalwale aliibua masuali kuhusiana na ukarabati wa afisi ya kaunti.
Share This Article