Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu ardhi imekamilisha kikao cha siku mbili katika eneo la pwani kutathimini bajeti ya afisi za usajili wa ardhi eneo hilo.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mugirango kaskazini Joash Nyamoko, ikiandamana na maafisa kutoka Wizara ya ardhi na mpiango ,ilizuru afisi za usajili ardhi katika kauntiya Kilifi kukagua ukarabati unaoendelea.
Badaye kamati hiyo ilifanya uchunguzi wa kubaini ukweli kuhusu shamba la ekari 417 linalozaniwa kati ya makundi ya washtaki waliowasilisha kesi mahakamani na mstawishaji wa kibinafsi.
Kundi la washtaki lilikutana na kamati hiyo ya bunge pamoja na wanachama kadhaaa kutoka jamii ya Magarini waliotaka kubaini ukweli, kuhusu umiliki wa shamba lenya utata la Galana Kulalu mpakani mwa kaunti za Kilifi na Tana River.