Kiongozi wa chama cha Wyper Kalonzo Musyoka na Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti, wamemshutumu Rais William Ruto kwa ubomozi uliotekelezwa katika shamba lenye utata linalomilikiwa na kampuni ya East Africa Portland Cement eneo la Mavoko kaunti ya Machakos.
Wakizungumza siku ya Jumamosi kwenye halfa ya kuchangisha pesa kwa ujenzi wa kaniza katoliki eneo la Katangi eneo bunge la Yatta ,Wavinya na Kalonzo walitaja kitendo hicho cha ubomozi kuwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Wavinya alikariri kumkampeinia Kalonzo katika eneo lote la Ukambani kuwania kiti cha Urais mwaka 2027.
Kalonzo alikashifu ubomozi huo na kuishutumu serikali kwa kudorara kwa uchumi wa nchini.