Kalonzo ataka kuachiliwa huru kwa vijana waliotekwa nyara

Dismas Otuke
1 Min Read

Viongozi wa upinzani wameitaka serikali kuwaachilia huru vijana wanaodaiwa kutekwa nyara na polisi.

Akiwatubia wanahabari  jijini Nairobi, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akiandama na wanasiasa wengine wameitaka serikali kuwaachilia huru watu waliotekwa nyara.

Kalonzo amesema kuwa watu 82 wametoweka katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita huku akiitaka serikali kuwaachilia huru.

Aliongeza kuwa inasikitisha kuona baadhi ya polisi waliovalia barakoa wakinaswa kwenye kamera za CCTV.

Haya yanajiri huku polisi wakiwarushia vitoza machozi waandamanaji waliofika katikati ya jiji kuandamana siku ya Jumatatu.

Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Kibinadamu, KNCHR imeripoti kuwa Wakenya 82 wametekwa nyara tangu mwezi Juni mwaka huu.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *