Yamkini watu kadhaa waliuawa kwenye vurumai na makabiliano yaliyoshuhudiwa nchini Tanzania siku ya uchaguzi mkuu jana Jumatano.
Aidha, serikali ilikatiza huduma za Intaneti huku mamia ya waandamanaji
wakikamatwa na jeshi la polisi.
Waaandamanaji wengi waliteta hatua ya Rais Samia Suluhu ya kukandamiza
upinzani.
Malalamishi yao ikiwa ni pamoja na hatua ya Rais Suluhu kumfunga kiongozi wa upinzani wa chama cha CHADEMA
ambaye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini.