Timu ya taifa ya Kenya kwa wasicha chini ya umri wa miaka 17 ,imeendeleza mazoezi yake katika Jamhuri ya Dominica, kujiandaa kwa makala ya nane ya fainali za Kombe la Dunia .
Kenya maarufu kama Rising Starlets ,watachezea mechi zao mjini Santiago de los Caballeros ,wakifungua kampeini kundini C dhidi ya Uingereza Oktoba 17 ,kabla ya kuikabili Korea Kusini tarehe 20 mwezi huu, na kumaliza mechi za makundi dhidi ya Mexico siku tatu baadaye.
Starlets waliwasili Dominican Jumatano lililopita baada ya kupiga kambi ya maozezi kwa wiki mbili nchini Uhispania.
Fainali za kombe la Dunia ambazo Kenya wanaofunzwa na Mildred Cheche wanashiriki kwa mara ya kwanza ,zitaandaliwa baina ya Oktoba 16 na Novemba 3 mwaka huu.