Junior Starlets waikwatua Uganda 3-0 na kufuzu kwa raundi ya tatu dhidi Cameroon

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 imefuzu kwa raundi ya tatu ya kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia, baada ya kuilaza Uganda mabao  3-0, leo katika marudio ya raundi ya pili uwanjani Nyayo.

Wenyeji Kenya walichukua uongozi kunako dakika ya 5 kupitia kwa Patience Ayieko kabla ya Brenda Achieng kuongeza mawili.

Junior Starlets wamefuzu kwa raundi ya tatu kwa ushindi wa jumla wa mabaoa 5-0 ,baada ya kuwashinda Uganda 2-0 kwenye duru ya kwanza wiki jana jijini Kampala.

Kenya chini ya ukufunzi wa Mildred Cheche inalenga kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mtawalia baada ya kushiriki mwaka jana katika Jamhuri ya Dominika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *