Junior Starlets waibwaga Dominica, mechi ya kirafiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wachezaji soka walio chini ya umri wa miaka 17 -Junior Starlets, waliwagutusha wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia jamhuri ya Dominica  walipowalabua magoli 3-1 jana katika mechi ya kujipima nguvu.

Starlets waliingoza kipindi cha kwanza mabao 2-0 kufikia mapumzikono Valerie Nekesa na Marion Serenge wakipachika goli moja kila mmoja,kabla ya Lindey Atieno kukongomelea msumari wa mwisho kwenye jahazi la Dominica kwa bao la tatu.

Kenya imeshinda mechi mbili na kutoka sare katika michuano mitatu ya kujipiga msasa.

Kenya inayoshiriki kipute cha Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza itafungua hekaheka  za kundi C dhidi ya Uingereza Oktoba 18, kabla ya kukabana koo na Korea Kaskazini tarehe 20 mwezi ujao.

Vidosho hao chini ya ukufunzi wa Midred Cheche, watahitimisha mechi za makundi kwa kugaragazana na Mexico tarehe 24 mwezi ujao.

Junior Starlets ni timu ya kwanza ya Kenya ya soka kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia.

Website |  + posts
Share This Article