Jumatatu tarehe 31 mwezi huu wa Machi, imetangazwa kuwa siku ya mapumziko kusherehekea siku kuu ya Idd-ul-Fitr.
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen ametangaza leo kupitia kwa gazeti rasmi la serikali.
Idd-ul-Fitr husherehekewa na Waislamu kuadhimisha kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.