Julien Alfred ampiga dafrao Richards na kutwaa dhahabu ya Olimpiki mita 100

Dismas Otuke
1 Min Read

Julien Alfred wa kutoka Saint Lucia ndiye bingwa mpya wa Olimpiki katika mita 100, baada ya kumshangaza bingwa wa Dunia Sha’ Carri Richardson wa Marekani Jumamosi usiku.

Alfred aliyekuwa amenyakua dhahabu ya mita 60 mashindano ya dunia ya ukumbini mwaka huu, alifyatuka uwanjani Stade De France na kuponyoka na dhahabu kwa sekunde 10.72.

Richardson aliridhika na nishani ya fedha kwa sekunde 10.87, huku Mellisa Jefferson wa Marekani, akishinda shaba kwa sekunde 10.92.

Mwnariadha huyo ndiye wa kwanza kutoka kisiwani Saint Lucia kunyakua medali katika michezo ya Olimpiki.

Awali kulikuwa na  utata baada ya Shelly Ann Fraser Pryce wa Jamaica kukosa kushiriki semi fainali  .

 

Share This Article