Jukwa la wanawake wasomi wa Afrika laandaa kikao na washikadau Kajiado

Tom Mathinji
2 Min Read

Jukwa la wanawake wasomi wa Afrika tawi la Kenya-FAWEK, kwa ushirikiano na washikadau wa kaunti ya Kajiado,lime a’ndaa kikao cha kujadili mikakati ya kuwarudisha shuleni wasichana waliojifungua wakiwa shuleni kama inavyo takiwa na serikali.

Kikao hicho ambacho kiliandaliwa kwenye kaunti ya Kajiado kwa lengo la kumaliza tabia za wasichana kupata mimba za mapema na kuacha masomo kutokana na mimba za mapema, kilihusisha wizara ya elimu, jinsia, afya, usalama na wazee wa jamii.

Kwa mujibu wa mshirikishi wa jukua hilo katika kaunti hiyo Nelly Naserian,jukwa hilo limefanya mengi makuu kwa lengo la kupiga jeki elimu ya mtoto wa kike.

Naye mkurugenzi wa jinsia wa kaunti hiyo, Catherine Mutinda,ameongeza kuwa itakuwa vema iwapo washikadau wote wataungana ili kufikia malengo hayo.

“ili sisi kupunguza hivi visa hadi sufuri, hatuwezi sema itafanywa na idara moja au mshikadau mmoja. Hivyo basi, tunarai kila mmoja kulipa kipaumbele na kuleta kila mshikadau kutoka jamii zote ili tuje pamoja kama timu na kuona kupungua kwa mimba za vijana na kuacha shule.” Alisema mutinda.

Katika harakati hizi, kaunti ya kajiado imebuni sehemu maalumu na salama eneo la Kitengela kwa wasichana walio jifungua kwa lengo la kulea wanao, kuendelea kielimu na kuepuka unyanyapaa.

Muchakato huo pia unalenga wavulana ambao wametelekezwa.

Share This Article