Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amemteua Judith Suminwa Tuluka, kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kama njia ya kutimiza ahadi yake wakati wa kampeini alipoahidi kuleta uswa wa kijinsia.
Bi Suminwa ambaye ni Waziri wa zamani wa mipango , anakabliwa na majumu magumu wakati taifa hilo linakabiliwa na msukosuko wa kisiasa hususan eneo la mashariki ambalo limekuwa na vita vya mara kwa mara licha ya kuwa na madini mengi.
Kwenye hotuba yake ya kwanza siku ya Jumatatu Waziri Mkuu huyo mpya, aliahidi kutoa kipa umbele kusuluhisha mizozo na kuleta amani.
Uteuzi huo unajiri wakati ambapo Congo inakabiliwa na changamoto nyingi tangu Rais Tshisekedi ashinde muhula wa pili.