JSC yaanza mchakato wa kujaza wadhifa wa Msajili Mkuu wa Mahakama

Tom Mathinji
1 Min Read
Tume ya JSC yawasaili watu saba kujaza nafasi ya msajili mkuu wa mahakama.

Tume ya huduma za mahakama (JSC), imeanza zoezi la kuwasaili watu saba waliopendekezwa kuteuliwa katika wadhifa wa msajali mkuu wa mahakama.

Saba hao walichaguliwa kutoka kwa orodha ya watu 47 waliotuma maombi kwa wadhifa huo, baada ya kipindi cha kuhudumu cha aliyekuwa msajili mkuu wa mahakama Anne Amadi kukamilika.

Saba hao ni pamoja na Macharia Rose Wachuka, Ouma jack Busalile, Mokaya Frida Boyani, Wambeti Ann Ireri, Ndemo Paul Maina, Kendagor Caroline Jepyegen na Kandet Kennedy Lenkamai.

Amadi alihudumu katika wadhifa huo kwa miaka 10, tangu mwezi Januari mwaka 2014. Wadhifa huo kwa sasa unashikiliwa na naibu msajili wa mahakama Paul Ndemo, ambaye pia anawania wadhifa huo.

Ndemo amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano. Jukumu la Msajili mkuu wa mahakama ni pamoja na kuandaa makadirio ya matumizi, kusimamia hazina ya mahakama kando na kuwa katibu wa tume ya huduma za mahakama.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article