Jose Chameleone na kakake walazwa hospitalini Amerika

Marion Bosire
1 Min Read

Baba ya mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Gerald Mayanja amethibitisha habari kwamba wanawe wawili, Jose Chameleone na Humphrey, wamelazwa hospitalini nchini Amerika.

Mzee huyo alikuwa akihojiwa na kituo kimoja cha habari nchini Uganda ambapo alisema kwamba wamekuwa wakipitia changamoto nyingi kama familia. Kulingana naye Chameleone amekuwa akiugua kwa miezi kadhaa sasa na hali yake inazidi kuzorota tangu ahamie Amerika.

Mayanja analaumu watu wenye nia mbaya hasa mitandaoni kwa mabaya yanayofika watoto wake. Kulingana naye, watu hao wanasema wanataka familia hiyo ya wanamuziki ianguke ndiposa wengine nao waweze kuinuka kimuziki nchini Uganda. “Kama humpendi mtu Mungu anampenda.” alilalama mzee huyo.

Kakake Jose Chameleone aitwaye Humphrey naye alichapisha picha akiwa amelazwa hospitalini huko huko Amerika. Alielezea kwamba alianza kujihisi mgonjwa akiwa safarini kuingia Amerika. “Nikiwa kwenye uwanja wa ndege wa Schiphol nilijipata nasinzia kila mara na kuhisi vibaya namna ambavyo sijawahi kuhisi.” alielezea Humphrey.

Baada ya masaa 10 alisafiri hadi uwanja wa ndege wa Logan akaelekea nyumbani ambapo aliingia na kulala. Alipoamka alipata kwamba tumbo lake lilikuwa likifura huku likiuma kiasi cha kutoweza kula chochote au kutembea. Alimwita rafiki yake ambaye alimpeleka hospitali ambako amelazwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *