Jopokazi la klabu ya AFC Leopards limeanza ziara yake nchini Tanzania katika klabu ya Yanga, leo kutathmini mbinu bora za kubadilisha timu hiyo ya ingwe kutoka klabu ya kijamii hadi shirika.
Jopokazi hilo linaloongozwa na mwenyekiti Dan Shikanda pia linajumuisha wanachama wengine Vincent Shimoli, Richard Ekhalie na Laureen Aseka.
Katika Zaira yao wamekutana na Rais wa klabu ya Yanga Hersi Said.
Leopards imo mbioni kuwa klabu ya kwanza ya kijamii nchini kubadilisha na kuwa kampuni kama njia ya kujitegemea kifedha.
Jokopokazi hilo pia litazuru klabu ya Simba na baadaye kuchukua maoni kutoka wanachama wa matawi yote nchini ,kabla ya ripoti hiyo kuwasilishwa kwa kamati kuu ya klabu hicho.