John Kiboko mmoja wa waliopigania uhuru kuzikwa Ijumaa

Marion Bosire
1 Min Read

Mwili wa John Kiboko ambaye ni mmoja wa waliopigania uhuru wa taifa la Kenya, utazikwa nyumbani kwake huko Ngorika katika kaunti ya Nyandarua Ijumaa Agosti 25, 2023.

Gavana wa kaunti ya Nyandarua Dr. Kiarie Badilisha alitangaza hayo baada ya kuzuru familia ya marehemu Jumapili.

Alisema serikali ya kaunti ya Nyandarua na serikali ya kitaifa zishirikiana kulipa bili ya hospitali ya shilingi milioni 8.2 iliyoachwa na Kiboko.

Badilisha alisema naibu rais Rigathi Gachagua amemhakikishia kwamba atahudhuria hafla hiyo ya mazishi.

Brigadier John Kiboko ambaye alikuwa kwenye kundi la Mau Mau alikata roho akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi Ijumaa Agosti 18, 2023, saa tano asubuhi.

Kifo chake kimejiri kabla ya kutekelezwa kwa mpango wa wana Mau Mau wa kutafuta na kufukua mabaki ya shijaa wa Mau Mau Dedan Kimathi kwa maziko ya heshima.

Mwakilishi wa wadi ya Kanjuiri Thuo Gachino ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya Kiboko, aliomba viongozi waliochaguliwa wa kaunti ya Kiambu wajitokeze kusaidia familia ya marehemu kugharamia mazishi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *