Jeshi la Wanamaji kusherehekea miaka 60 leo

Dismas Otuke
1 Min Read

Jeshi la Wanamaji litasherehekea miaka 60 leo tangu kubuniwa kwake Disemba 14 mwaka 1964.

Hafla hiyo itakayoandaliwa katika makao makuu ya jeshi la Wanamaji eneo la Mtongwe Feri,itahudhuriwa na Rais William Ruto.

Kama sehemu ya maandalizi ya sherehe hizo wanajeshi hao wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya, walifanya zoezi la upanzi wa miti katika juhudi za kuafikia ruwaza ya serikali kupanda mti bilioni 15 ifikiapo mwaka 2032.

Jumla ya miche 60,000 ya mikoko ilipandwa kuambatana na sherehe za leo za miaka 60.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *